Meneja wa klabu ya West Ham Utd Slaven Bilic, amepinga maamuzi ya mwamuzi Mike Dean aliyechezesha mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo kati ya kikosi chake dhidi ya Man Utd.

Katika mchezo huo Man Utd waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, yakifungwa na Juan Mata na Zlatan Ibrahimovich katika dakika ya 63 na 78.

Bilic amesema kiuhalishia mwamuzi Dean hakuitendea haki West Ham Utd, kutokana na udhaifu mkubwa aliouonyesha huku akidai aliwabeba makusudi Man Utd.

Dean ambaye tayari ameshatoa kadi za njano tano katika michezo 15, alimuadhibu mshambuliaji wa The Hammers Sofiane Feghouli kwa kumuonyesha kadi nyekundu kufuatia rafu aliyomchezea beki wa Man utd Phil Jones.

Uamuazi wa mchezaji huyo kupewa kadi nyekundu umepingwa na Bilic kwa kusema haikupaswa kutolewa adhabu kama hiyo kutokana na uzito wa kosa lililotendeka, ambapo amedai wachezaji hao wawili walikua katika hali ya kuwania mpira hivyo kwa maono yake ilikua ni 50-50.

Feghouli alikumbana na adhabu hiyo katika dakika ya 15, hali ambayo ilikifanya kikosi cha West Ham Utd kucheza pungufu kwa dakika 75 za mchezo.

Lawama nyingine ambayo Bilic amemtupia mwamuzi Dean ni kuhusu bao la pili la Man utd ambalo lilifungwa na Zlatan Ibrahimovic, ambapo amesema mshambuliaji huyo alikua ameotea kabla ya kufanya maamuzi ya kupiga mpira langoni mwa West Ham Utd.

Hata hivyo Bilic amesisitiza kukata rufaa kupinga maamuzi ya kadi aliyoonyeshwa mchezaji wake kwa akuamini alionewa makusudi.

Kwa matokeo hayo Man Utd wamefikisha point 39 wakiendelea kukaa kwenye nafasi ya sita huku West Ham Utd wakiwa kwenye nafasi ta 13 kwa kumiliki point 22.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini England iliyochezwa jana.

Middlesbrough 0-0 Leicester City

Everton 3-0 Southampton

Manchester City 2-1 Burnley

Sunderland 2-2 Liverpool

West Bromwich Albion 3-1 Hull City

 

Leo ligi hiyo inaendelea tena ambapo

Bournemouth v Arsenal

Crystal Palace Vs Swansea City

Stoke City v Watford

Guardiola: Nakaribia Kustaafu Kufundisha Soka
Azam FC Yakusanya Point Tatu Zanzibar