Bilionea, Mustapha Jaffer Sabodo ametangaza kuunga mkono juhudu za Rais John Magufuli kuhamishia Serikali yote mkoani Dodoma, akiahidi kuwekeza dola milioni 5 (sawa na shilingi trilioni 11) katika huduma mbalimbali za jamii mjini humo.

Sabodo ameweka wazi mpango huo jana akieleza kuwa amefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kuhamishia Serikali Dodoma akieleza kuwa aliposikia uamuzi huo alitabasamu moyoni kwani aliona roho ya Mwalimu Julius Nyerere imezaliwa upya.

“Kwa hiyo natangaza kuunga mkono Azimo la Dodoma kwa kuwekeza dola za Marekani bilioni 5, ambazo zitatumika kwa ajili ya uwekezaji mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani humo,” alisema Sabodo.

Sabodo ameongeza kuwa atawashawishi wafanyabiashara wakubwa wa Singapore na India kuwekeza Dodoma. Alisema kwa kuanza ataishawishi hospitali ya Apollo kuwekeza katika huduma za afya mkoani humo na mikoa ya jirani ili kupata huduma hiyo kwa kiwango cha kisasa.

Sambamba na uamuzi huo, Sabodo ametangaza kusitisha kukisaidia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho amekuwa akikisaidia kwa muda mrefu kifedha.

“Huko nyuma nilikuwa nawapa Chadema fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuimarisha demokrasia, sasa natangaza tena kwamba sitawapa tena fedha, niwape za nini wakati Rais aliyeko madarakani anafanya kazi ambayo ndio nilikuwa naipigania?”  alihoji.

Alisema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais magufuli hususan katika kupambana na rushwa na ufisadi nchini.

Donald Trump afyatuka, adai Clinton ni ‘Shetani’
Mrema alia na Paul Makonda kuhusu Bodaboda