Bilionea maarufu wa madawa ya kulevya wa Mexico, Joaquin Guzman maarufu kama El Chapo anayeshikiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali baada ya kutoroka mara mbili gerezani, ametoa kilio chake kuhusu kinachomsibu ndani ya mahabusu.

Mwanasheria wa El Chapo anayefahamika kwa jina la José Refugio Rodríguez amesema kuwa mteja wake alimsimulia kuhusu kinachomsibu ndani ya mahabusu za gereza la Ciudad Juarez, akidai anaweza kupoteza kumbukumbu au hata kuwa kichaa.

El Chapo3

Elchapo baada ya kukamatwa

Alisema kuwa ujumbe aliopewa na El Chapo unaeleza kuwa anaona vitu ambayo vinamfanya ahisi anakaribia kufa.

Rodríguez anasema kuwa bilionea huyo amelalamika kuwa huamshwa kila baada ya saa nne kwa ajili ya ukaguzi, hali inayomfanya ashindwe kupata muda wa kusinzia hivyo yuko katika hatari ya kupoteza kumbukumbu.

“Aliniambia kuwa ‘hawaniruhusu kulala usingizi, sioni mwanga saa zote 24’,” alisema mwanasheria huyo ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha mteja wake hahamishiwi nchini Marekani.

Katika hatua nyingine, New York Post imeripoti kuwa mke wa El Chapo, Emma Coronel amelalamika katika Tume ya Haki za Binadamu kuhusu hali ya mumewe ambaye ni mtuhumiwa akidai kuwa anaweza kuwa kichaa muda wowote.

Emma Coronel

Emma Coronel

Mwanamke huyo pia analalamikia hatua za kupunguziwa muda wa kumtembelea mumewe na kuwa na faragha ya mapenzi kutoka saa nne kwa wiki mbili hadi saa mbili kwa wiki mbili.

Kauli ya Mashali kuhusu chanzo cha kupigwa kabla ya kufa yawekwa wazi, ”ni sh 1000!”
Nana Kwaku: Jose Mourinho Amuombe Radhi Eva Carneiro