Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombardier ndogo 1, pamoja na malipo ya bilioni 50 kwa ajili mradi wa kufua umeme wa katika bwawa la Julius Nyerere

Ameyasema hayo leo Septemba 4, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma pamoja na kupokea na kujibu maswali ya wananchi waliokuwa wakipiga simu.

“Serikali imefanya malipo ya awali ya ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombadier ndogo 1, pia serikali imefanya malipo ya bilioni 50 kwenye mradi wa reli na bilioni 50 kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere,” amesema Msigwa.

Nandy kuisimamisha Dar viwanja vya posta
Waziri Lukuvi ataka maonesho ya kimataifa ya Teknolojia ya ujenzi wa nyumba