Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, chini ya Wakala wa Ufundi na umeme Tanzania TEMESA imetenga fedha kiasi Cha shillingi Bilioni 6.3 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwaajili ya kuvifanyia ukarabati vivuko Nchini ambavyo vimefikiwa muda wake wa kukarabatiwa

Hayo yamesemwa leo wakati wa mapokezi ya Kivuko Cha MV Mafanikio kilichorejea kutoa huduma Mkoani Mtwara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake uliochulua takriban miezi miwili na nusu

Akizunguma na wananchi waliofika kushuhudia tukio la upokeaji wa kivuko hicho lililofanyika katika eneo la Msemo Shangani Mjini Mtwara katika kivuko cha Msangamkuu – Msemo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amesema ni utaratibu wa kawaida kwa Serikali kuvifanyia vivuko ukarabati kila inapopita miaka minne hadi mitano ili kuviwezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, amesema ukarabati wa kivuko cha MV. MAFANIKIO umefanywa na kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Ltd. Boat Yard ya jijini Mwanza kwa gharama ya shillingi milioni 493.6

‘’Baadhi ya kazi zilizofanyika katika ukarabati huu ni pamoja na Kuweka deki mpya ya magari, kuweka milango mipya miwili (2-New ferry ramps), kuweka ramp lifting cylinder cover mpya, kutengeneza mifumo ya steering, propulsion pamoja na injini na kupaka rangi kivuko chote.’’ Amesema Mhandisi Maselle.

Aidha vivuko vitakavyokarabatiwa ni pamoja na MV. Kitunda (Lindi), MV Tanga (Pangani Tanga), MV Kazi na MV magogoni (Dar es salaam), MV Ruhuhu (Ruvuma) pamoja na vivuko vinavyofanya kazi kwenye ziwa Victoria ambapo amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwa ajili ya ukarabati wa vivuko hivyo.

Kivuko cha MV. MAFANIKIO kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari sita sawa na tani 50 na kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya pamoja na wananchi wakazi wa Msangamkuu na Msemo wakishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MAFANIKIO baada ya kukipanda ambapo kiliwapeleka upande wa Msangamkuu na kurudi Msemo baada ya kupokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70 na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Msemo Shangani katika kivuko cha Msangamkuu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akimuonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti wakati walipokuwa wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO ambacho kimepokelewa leo na Mkuu huyo wa Mkoa. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70 na tayari kimeanza kutoa huduma. Kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wakijadiliana jambo mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kupokea rasmi kivuko cha MV. MAFANIKIO katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo la Msemo Shangani katika kivuko cha Msangamkuu. Kivuko hicho ambacho kinatoa huduma kati ya Msangamkuu na Msemo Mkoani Mtwara kimefanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 496,609,357.70.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kushoto akimuonyesha kitu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wakati walipokuwa wakikagua kivuko cha MV. MAFANIKIO mara baada ya kukipokea rasmi mapema leo katika hafla fupi iliyofanyika Mkoani Mtwara. Mbele yao ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya na Mkurugenzi wa vivuko wa Wakala huo Mhandisi Adelard Kweka.

Majaliwa atoa maagizo kwa wakuu wa mikoa
Bidhaa muhimu kukosekana Sudan