Waziri wa Madini Mhe. Dkt Dotto Biteko ameliomba Bunge kupitisha Makadirio ya shilingi bilioni 83,445,260,000.0 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Bungeni Dodoma Dkt. Biteko amesema fecha hizo ni kwa jailli ya Wizara kutekeleza majukumu na malengo yaliyopangwa.

Katika Fedha hizo zilizoombwa na Wizara ya Madini, Shilingi 22,000,000,000.0 ni fedha za maendeleo, Shilingi 61,445,260,000.0 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Kati ya hizo, hilingi 20,609,600,000.0 ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi 40,835,660,000.0 ni matumizi Mengineyo.

Dkt. Biteko amesema Wizara pamoja na taasisi zake zina lengo la kuendelea kuimarisha sekta nzima ya Madini ili kuendelea kuongeza pato la taifa.

“Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha uwezo wa Taasisi katika kutoa huduma, GST inakusudia kufanya yafuatayo: kuboresha mifumo ya uchakataji, uhifadhi na usambazaji wa taarifa za jiosayansi kuhusu upatikanaji wa madini; kuwawezesha watumishi kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu; kuboresha mazingira ya utendaji kazi na maslahi ya watumishi; kutangaza (marketing) bidhaa na huduma zitolewazo na GST; na kukamilisha kufanya mapitio na maboresho ya Muundo wa Taasisi ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya GST,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema Tume ya Madini itaendelea kuzihusisha mamlaka nyingine za Serikali zinazofungamana na sekta katika utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Taasisi za Fedha, pamoja na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha changamoto mbalimbali zikiwemo za kisheria, mitaji, upatikanaji wa vibali, tozo na kodi ambazo zimekuwa zikiwakabili wachimbaji nchini zinatatuliwa kwa wakati na kwa maridhiano.

“Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Tume ya Madini imefanikiwa kutoa leseni 2 za uchimbaji wa Mkubwa wa Madini ya Dhahabu, na Uchumi wa Madini chini unatokana na Madini ya Dhahabu ambayo huchangia takribani asilimia 80 ya mapato yatokanayo na rasilimali ya Madini,” amesema Dkt. Biteko.

Baada ya kueleza mipango yote ambayo Wizara yake imepanga kutekeleza kwa Mwaka wa fedha 2022/2023, Waziri Dkt. Biteko aliomba Bunge idhini ya kupitisha bajeti ya shillingi Bilioni 83.4.

Hayati Kibaki aagwa kitaifa nchini Kenya
Ajabu, Mpangaji ataka kumdhulumu nyumba mmiliki wake!