Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amelazwa katika Hospitali ya Irvine ya Chuo Kikuu cha California na kuwekwa katika chumba cha uangalizi wa dharura (ICU).

Daktari wake aliiambia CNN jana jioni kuwa Clinton ana tatizo katika mfumo wa mkojo ambapo madhara (infection) yamesambaa kwenye mfumo wa damu.

Hata hivyo, amesema kuwa Clinton anaendelea vizuri na kwamba anaweza kuzungumza na ndugu na jamaa, pia anaweza kusimama mwenyewe.

“Baada ya siku mbili za matibabu, tunaona seli nyeupe za damu zinaenda vizuri na matibabu anayoyapata yanamsaidia vizuri. Tunategemea ataruhusiwa kutoka hospitalini hivi karibuni,” daktari wake alisema.

Taarifa iliyotolewa na ofisi yake imeeleza kuwa Clinton alikuwa California kwa ajili ya tukio binafsi, lakini alianza kusikia vibaya na kuamua kwenda kupima. Baada ya vipimo, alilazimika kulazwa kwa ajili ya hatua zaidi za matibabu.

CAF yalegeza masharti, Mashabiki rukhsa
Kenyatta akutana na Biden, wajadili haya