Rapa Billnas amethibitisha kuwa mkewe ambaye ni mwimbaji mahiri wa muziki wa Bongo fleva Nandy amefanikiwa kujifungua mtoto wa kike akiwa salama na mwenye afya njema.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Billnas amechapisha taarifa hiyo iliyoambatana na ujumbe mrefu akithibitisha kujifungua kwa mkewe, ukiambatana na shukurani zake za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kumpokea mtoto wao wa kwanza.

“Ahsante Mungu Kwa zawadi na Baraka…kila iitwapo leo!! Kwangu Mimi 2022 ni mwaka wa kipekee sana…nina kila sababu ya kushukuru na Kutoa Sadaka, Mungu wetu ni mwema Sana, Pili kipekee Niseme Ahsante mke wangu kipenzi Nandy kwa kuniletea Mrembo na Rafiki.

Haikuwa kazi rahisi umenionesha wewe ni shujaa kiasi gani kuanzia Mtoto akiwa tumboni mpaka muda unajifungua umepigana sana nimejionea namna gani mtu anaweza ku risk kupoteza uhai wake wakati wa kujifungua.

Hii imefanya nizidi kukupenda, Kukuheshimu na kukupa nafasi ya pekee katika maisha yangu, Hayo yote hayatoshi lakini kila siku nakuombea Kwa Mungu akulinde mke wangu na nitakupa furaha na kufanya maisha yako yawe ya Amani kwani Unastahili Mengi Mazuri.

Sina zawadi kubwa itakayoweza lingana na upendo wangu kwako zaidi ya kuzidisha upendo kila iitwapo leo, nikuhakikishe uko Mikono Salama.

Tatu kwa mwanangu kipenzi Najuwa ipo siku utakuja kuisoma hii, Niseme tu nakupenda sana sana na umekuja na baraka nyingi ambazo siwezi hata kuzieleze, Mwenyezi Mungu akutunze kwa Mapenzi yake na Ukawe mtu mwema katika ulimwengu wa kawaida na wa kiroho”. Amendiaka Billnas.

Billnas na Nandy walifanikiwa kuingia kwenye maisha ya ndoa rasmi ndoa Julai 16, 2022.

Kenya: Wakili wa Odinga asema IEBC haiwezi kuaminiwa
Marekani yasimama 'Made in Lagos' ya Wizkid