Nyota wa muziki nchini, Billnass ameandika historia mpya jana April 10, 2020 mbele ya watazamaji wa show ya Homa inayoendeshwa na kituo cha televisheni cha E baada ya kuamua kumvisha pete ya uchumba Faustina Mfinanga maarufu kama Nandy na kudai kuwa jambo hilo lilimchukua muda wa wiki moja kulipanga na kulikamilisha.

Ambapo Billnass amesema kuwa kama ingekuwa hiyari yake angeweza kumuoa Nandy mapema iwezekanavyo hata kabla ya jumapili kufika au hata usiku huo huo aliomvalisha pete.

Alipokuwa akihojiwa amesema kuwa uamuzi huo ulikuwa siri kubwa kwani hata wazazi wa pande zote mbili hawakuwa na taarifa juu ya jambo hilo la kheri kwani alitaka liwe la mshangao mkubwa kwa mpenzi wake Nandy.

Billnas amesema Nandy ni mwanamke sahihi kwake ndiyo maana ameamua kumpeleka hatua nyingine ya mahusiano yao na anampenda sana Nandy na anataka awe tayari kwani kwa sasa ni mke wa mtu mtarajiwa hivyo anapaswa kuyachukulia kwa makini mahusiano hayo ili wafikie malengo yao ya kufunga pingu za maisha kwani changamoto katika maisha zipo hususani kwao ambao ni wasanii wadogo.

Aidha wakati Billnass anamvalisha pete alisikika akizungumza maneno haya yanayoashiria upendo, wameshibana na kujuana kwa pande zote nzuri na pande mbaya na tayari wamefikia hatua ya kuweza kuishi pamoja kama mume na mke.

”We have been together kwa kipindi kirefu sana, tumepitia vitu, vizuri na vibaya, najua upande wako mbaya najua upande wako mzuri, but nimechagua pande zote mbili, Nakupenda sana” amesema Billnass.

Tanzia: Wafanyakazi wawili TBC wafariki dunia
Mbowe amuangukia Magufuli hatma ya watanzania na Corona

Comments

comments