Mwanamuxiki was hip hop Billnass s amesema kuwa Sasa hivi amekuwa anapitwa na vitu vingi sana ambavyo vinanaendelea katika mitandaoni kijamii, kwa sababu ya kuacha kutumia simu mara kwa mara.

Billnass amesema hayo baada ya kuulizwa Kama ameiona video ya msanii Rosa Ree,  ikionyesha anashikwa maungo ya kifuani kwenye mwili wake.

“Mimi muda mwingine napitwa na vitu vingi sana, kwa sababu zamani nilikuwa na tatizo la kuwa “addicted” na simu, muda wote nashika simu kwa hiyo sasa hivi najitahidi na naweza nikakaa siku nzima nikazima simu kwa hiyo muda mwingine napitwa na vitu” amesema Billnass

Aidha ameendelea kwa kusema anafanya hivyo ili kujirudisha katika hali ya kawaida, kwa sababu muda mwingine simu zinaweza zikafanya kazi zisiende na vitu vingine.

Video hiyo ya Rosa Ree imeshafutwa katika mtandao wa YouTube pia amefungiwa kwa muda wa miezi sita kutofanya kazi za sanaa na faini ya Milioni 6 kutoka kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya kutoa video isiyo na maadili.

Mmarekani mweusi wa kwanza kuwekewa uso bandia
Mkapa alivyokataa sura yake kuwekwa kwenye fedha

Comments

comments