Malipo ya Bima ya Maisha kwa Marubani wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air, iliyotokea mjini Bukoba mkoani Kagera na kupoteza Watu 19 yamelipwa na Kampuni ya Alliance Life Assurance Ltd.

Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Life Byford Mutimusakwa ameamesema malipo hayo yatazisaidia familia za Marubani hao kuendeleza kile yale yaliyokuwa yakifanywa na wapendwa wao huku akitoa wito kwa umma kuhusu umuhimu wa kuwa na Bima za Maisha.

Ndege ya Shirika la Precision Air iliyopata ajali Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kuokolewa.

Katika hotuba yake baada ya kupokea hundi ya mafao hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Patrick Mwanri aliwashukuru Alliance Life kwa uharaka wa malipo ya madai ya Marubani hao.

Ajali hiyo ya ndege ya Precion Air ilitokea Novemba 6, 2022 na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 24 kuokolewa huku wadau wakihoji mambo mengi ambayo hata hivyo ilibidi kusubiri ripoti rasmi za mamlaka.

Serikali kuendeleza usimamiaji ilani ya CCM
Makamu wa Rais Equinor atembelea eneo la ujenzi mradi LNG