Binti wa Rais wa Congo, Jullienne Sassou Nguesso anatuhumiwa kula rushwa huku mali zake  nchini Ufaransa zikichunguzwa.

Jullienne Nguesso na mumewe Guy Johnson wiki hii wamewekwa chini ya ulinzi nchini Ufaransa huku mali zao zikichunguzwa kwa tuhuma za utakatishaji wa fedha na matumizi mabaya.

Aidha, hatua hiyo imefikiwa mara baada ya watu hao wawili kununua jumba la kifahari Jijini Paris katika kitongoji maarufu cha Neuillysur-Seine kilichopo kaskazini mwa jiji hilo.

Wachunguzi wa mali hizo za Jullienne na mumewe wamesema kuwa wamegundua kiasi kikubwa cha mamilioni ya fedha za Serikali yalihamishwa kutoka Congo Brazaville tangu mwaka 2007 na kuingizwa kwenye akaunti za kigeni nchini Ushelisheli, Kisiwa cha Mauritius na Hong kong.

Hata hivyo, maafisa upelelezi nchini Ufaransa wanauchunguza ukoo mzima wa Sassou Nguesso na jamaa za Omar Bongo ambaye ni kiongozi wa Gaboni na raisi wa Teodoro, Obieng Nguema wa Guinea ya Ikweta.

 

 

Viongozi wa dini waombwa kukemea mauaji Pwani
Marekani yatoa wito kwa Qatar kumaliza mzozo na nchi za Kiarabu