Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Dotto Biteko amemuagiza Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kusini, Mayigi Makorobela kuanzisha haraka ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo kupeleka wataalamu ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo ikiwemo elimu ya usalama kazini.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

Amesema kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo ambapo alibaini kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali wa ofisi.

Aidha, ameongeza kuwa Waziri Mkuu anawapenda wachimbaji wadogo wadogo nchini ambao hata Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alibainisha kuwanufanisha Watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo madini.

“Mhe Rais Dkt. Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi kunufaika na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi iliporuhusu uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa Watanzania badala yake madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine,”amesema Biteko

 

 

Video: Kingunge, Maalim Seif wamjadili Lowassa, Mafuriko ya Kibaigwa yatia hofu wabunge
Magazeti ya Tanzania leo Januari 19, 2018