Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema kuwa hakuna tozo yeyote inayotozwa kwa wafanyabiashara wa dhahabu inayoingizwa nchini kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es salaam kwenye kikao cha Rais John Magufuli na wafantyabiashara, ambapo mfanyabiashara mmoja alilalamikia kitendo cha TRA mkoani Kigoma kutoza dolla 300 kwa wafanyabiashara wa dhahabu kutoka nchi za Kongo na Burundi

Amesema kuwa ni ruksa kwa wafanyabiashara ya dhahabu kutoka nchi za nje kuja nchini kuuza dhahabu zao, kwani mpaka sasa tayari nchi mbalimbali kama Zambia na Malawi wameshaanza kuuza nchini.

”Kwa malalamiko yaliyotolewa na mfanyabiashara kutoka Mkoani Kigoma kwakweli si sahihi, sheria haisemi hivyo kwamba mfanyabiashara wa dhahabu kutoka nje ya nchi atozwe dolla 300, hapana sisi tuanawahitaji sana hawa wafanyabiashara, sababu tumefungua masoko mengi sana lakini kama lipo lazima tulikomeshe.”amesema Biteko

Hata hivyo, waziri Biteko ameongeza kuwa wafanyabiashara wa dhahabu kutoka nchi za nje wanakaribishwa kuingia nchini kufanyabiashara ili kuweza kuipatia nchi mapato na kufikia uchumi wa kati.

Rais Museveni amuondoa Chameleon kwenye Twitter yake baada ya kutangaza kugombea
Msipowekeza kwenye maeneo mtanyang'anywa tu- Lukuvi