Kundi la muziki la Black eyed linatarajia kufanya onyesho kabambe la muziki katika fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya itakayopigwa leo mjini Cardiff kwenye uwanja wa taifa wa Wales.

Aidha, Black eyed peas wata shambulia jukwaa na kutoa burudani kwa mashabiki watakao hudhuria kwenye fainali hiyo inayozikutanisha miamba ya soka barani humo timu kotoka Hispania na Italia Real Madrid na Juventus.

“Tumepanga kutoa burudani ambayo haitasahaulika, kwani nafasi kama hii mara nyingi huwaga ni adimu kupatikana hivyo sisi kama kundi tutawafanya mashabiki wa mpira wa pande zote mbili kufurahi,”amesema William wa Black eyed peas.

Hata hivyo, katika mchezo huo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki

Picha mpya za Beyonce zazua gumzo, mashabiki waunganisha matukio
ANC wataka Rais Zuma achunguzwe tena, washindwa kumtetea