Filamu ya Black Panther iliyowakilisha uwezo wa waafrika katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na teknolojia, imeweka rekodi nyingine ya mauzo kwa kufikia $bilioni 1 sokoni.

Imeelezwa kuwa mauzo hayo yametokana na makadirio ya tiketi zilizouzwa. Taarifa hiyo ya mauzo imekuja ikiwa ni siku 26 tangu filamu hiyo ilipoachiwa rasmi.

Disney pia wamesema Black Panther imekuwa filamu ya tano kutoka kampuni ya Marvel Universe kufikisha mauzo ya $bilioni 1. Filamu nyingine zilizofikia mauzo hayo ni pamoja na The Avengers, Avengers: Age of Ultron, Iron Man 3, na Captain America: Civil War.

Filamu hiyo ambayo ndani yake kuna Mkenya, Lupita Nyong’o imepata umaarufu mkubwa na kuingiza $521 milioni ndani ya Marekani pekee na kushika nafasi ya 2, ikiipita The Dark Knight.

Black Panther imeongozwa na Ryan Coogler, wahusika wakuu ni Boseman na Michael B. Jordan pamoja na Lupita Nyong’o.

Mayweather kuzichapa ngumi na mateke, mkufunzi wake afunguka
Lissu kufanyiwa upasuaji wa 19, atuma ujumbe

Comments

comments