Timu ya Black Sailors (Mabaharia weusi) yenye maskani yake Magomeni Jitini ambayo inashiriki ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja kwa sasa ndio timu pekee ya Mitaani ambayo inafanya vizuri katika ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja wakiwa wana alama 25 kwasasa wakishika nafasi ya 3 kwenye msimamo.

Jana usiku walifanikiwa kuwafunga vinara wa ligi hiyo ambao pia ni wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika JKU , kwa bao 1-0 bao pekee lililofungwa na Abdul Azizi Seif (Ngasa) mchezo uliochezwa katika Dimba la Amaan.

Sailors ndio timu pekee kwa msimu huu ilowahi kuzifunga timu 2 wa kimataifa (Mafunzo na JKU) ambao ni bingwa mtetezi na Makamu wanaowakilisha Zanzibar katika mashindano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mbali ya rikodi hiyo pia Sailors inarikodi nyengine nzuri kuwa ndio timu pekee mpaka sasa imecheza michezo mitatu mfululizo bila ya lango lake kuruhusu kufungwa hata bao moja.

Michezo hiyo mitatu mfululizo Sailors ilicheza jana ikafanikiwa kuifunga JKU bao 1-0, mchezo mwengine walicheza tarehe 16/02/2016 na timu ya Polisi na walimaliza kwa sare ya 0-0, na tarehe 02/02/2016 Sailors walimfunga bingwa mtetezi Mafunzo mabao 3-0.

Hivyo imecheza michezo mitatu mfululizo pasipo kufungwa hata bao moja na hii inaonesha kuwa ina ulinzi imara kwasasa hasa baada ya kufanya usajili wa dirisha dogo.

Rikodi nyengine iloweka Sailors katika ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja mapka sasa haijawahi kufungwa na timu yoyote ya Mitaani kama vile Miembeni, Kimbunga, Mtende Rengers, Jangombe Boys, Kijichi na Chuoni.

Mbali na rikodi hiyo Sailors haijafungwa na timu zote za vikosi vya Muungano yani timu ya Polisi na wana Jeshi Kipanga ambapo katika michezo miwili waliokutana Sailors na Polisi , mmoja Sailors kashinda na mmoja sare wakati walipokutana na Kipanga mchezo mmoja Sailors 1-0 Kipanga.

BLACK SAILORS mpaka sasa imeshacheza michezo 15, ambapo imeshinda michezo 7, wameenda sare michezo 4 na kufungwa michezo 4, ambapo michezo yote hiyo waliopoteza mzunguko wa mwanzo wamefungwa na baadhi ya timu za Vikosi vya S.M.Z wakiwemo KVZ, JKU, KMKM na Zimamoto.

Black Sailors ilianzishwa tangu mwaka 1981 ambapo huu ndo msimu wake wa kwanza kucheza ligi kuu soka Zanzibar tangu kuanzishwa kwake na kwasasa inaonekanwa kuwa ni timu tishio kufuatia vipaji vingi alivyovisajili kocha mkuu wa timu hiyo  Juma Awadh wakiwemo Mustafa Vuai (JR) Fasihi Pina, Muharami Khamis (Tela), Omar Mahmoud (Waziri wa Ulinzi), Rajab Abdallah, Abdul Ali, Bakar Kuluzo, Iddi Idrissa, Majid Khamis (Mido Dudu), Ramadhan Wilson, Juma Machano (Kaseja), Abdul Azizi Seif (Ngasa), Nassor Salum, Ramadhan Hamad, Hassan Mkwabi, Salum Mjaka, Hassan Said (Kilahe), Abdallah Amour na wengine wengi tu wakishirikaina kwa pamoja na benji lao la Ufundi .

Wachezaji Wa Coastal Union Wawasha Moto Klabuni
Ligi Daraja la Pili (SDL) Kufikia Kikomo Mwishoni Mwa Juma