Aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Joseph Sepp Blatter na Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), Michel Platini watalazimika kukaa nje ya soka kwa kipindi cha miaka 8 baada ya kushushiwa rungu hilo na Kamati ya Maadili ya FIFA.

Kamati hiyo ya Maadili imewaamuru Blatter na Putini kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka 8 baada ya kuwakuta na hatia katika tuhuma mbalimbali za kifisadi na kimaadili zilizoelekezwa kwao.

Katika moja ya tuhuma walizokutwa na hatia viongozi hao wakuu wa soka ni pamoja kuhusika katika malipo yasiyo rasmi ya dola milioni mbili.

Hata hivyo, Blatter na Platini wameendelea kupinga tuhuma hizo na wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya maamuzi hayo.

Tayari msemaji wa Blatter amethibithibitisha kuwa atakata rufaa katika Mahakama ya usuluhisho wa masuala ya michezo.

Viongozi wa CCM wafungiwa ndani Kwa Saa Nne Kuwasaka Wasaliti
Madiwani wa CUF Kufikishwa Mahakamani Kwa Kufanya Vurugu