Rais wa Shirikisho la Soka duniani FIFA, Joseph Sepp Blatter, amelazwa hospitalini kutokana na kupatwa na mshituko wa moyo.

Blatter aliyesimamishwa kwa siku 90 kujishughulisha na masuala ya soka, kufuatia uchunguzi wa kashfa ya matumizi mabaya ta fedha za FIFA, alilazwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya lakini sasa imeelezwa ataendelea kubaki kwa uchunguzi zaidi.

Rais huyo aliyeongoza ulimwengu wa soka kwa miaka 18, awali ilidaiwa alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo hivyo ikabidi apate huduma ya matabibu, lakini alibainika ana matatizo ya mshtuko ya sasa imebainika ana tatizo la mshituko wa neva.

Awali, mwanasheria wa Blatter, Richard Cullen alieleza juu ya uangalizi huo wa madaktari, lakini akasema alitarajia arejee nyumbani mapema kabla hali kubadilika na kutolewa maelezo tofauti.

Hata hivyo, watu wake wa karibu wameeleza hali yake si mbaya na anatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida japokuwa atabaki hospitalini hadi mapema juma lijalo.

Msaidizi wake, Walter Gagg, amesema Blatter anatarajiwa kuwa mwenyeji wa hafla ya kukabidhi tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka 2015, ambazo zitafanyika januari 11 mwaka 2016.

Ancelotti: Nipo Tayari Kumpokea Mzigo Jose Mourinho
Lamine Diack Ajiweka Pembeni Kwa Kashfa