Kampuni ya BMW imezindua na kulionyesha gari la kwanza Duniani aina ya BMW iX Flow SUV lenye uwezo wa kubadilika rangi, likitumia teknolojia iitwayo E Ink ama ‘Wino wakielektroniki’.

Hii ni gari itakayompa uwezo mmiliki kubadilisha rangi ya nje ya gari hilo kwa namna atakavyo wakati wowote atakapohitaji kwa kubofya kitufe maalumu cha kubadilishia rangi na bila kuchukua muda, rangi ya gari hilo itabadilika papo hapo.

BMW iX Flow SUV ni gari ya umeme lililowekewa mfumo mwingine maalumu unaoweza kumuonyesha mmiliki kuwa imeisha au imejaa chaji kwa kiwamgo stahiki.

Licha ya ufahari wa kumiliki gari hilo, kwa mujibu wa Stella Clarke, mjumbe wa bodi ya usimamizi ya BMW AG, anasema kuwa hata ikitokea umeegesha gari hilo kwenye eneo lenye magari mengi yenye rangi moja kiasi cha kushindwa kulitambua gari lako kwa urahisi,
Basi kwa kutumia kitufe kilichopo kwenye remote maalumu ya gari hilo utaweza kuliona gari lako kwa kuliamuru libadilike rangi ili uweze kulitambua kwa urahisi.

“Kama unaweza kuchagua nguo unazovaa. Unachagua namna ya kuishi kwenye mitandao ya kijamii. Basi sasa unaweza kuchagua rangi ya gari lako,” alisema Stella Clarke, mjumbe wa bodi ya usimamizi ya BMW, katika taarifa.

Ripoti kutoka BMW ni kuwa gari hilo, bado kampuni hiyo haijawa tayari kuliingiza sokoni rasmi kwaajili ya kuuzwa na kwa sasa lipo katika majaribio kwa kuwa yapo mambo kadhaa yanayoendelea kuboreshwa zaidi.

Trippier akaribishwa Newcastle UTD
Milioni 346 kwa atayempata Muuaji wa Young Dolph