Rungu la sheria ya makosa ya mitandaoni limemuangukia mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu nchini Tanzania Chacha Wangwe, Bob Chacha Wangwe, kwa kuhukumiwa  kwenda jela mwaka mmoja na miezi sita au kulipa faini ya milioni 5.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, na mshtakiwa kutakiwa kutekeleza moja ya adhabu hizo alizoambiwa.

Aidha, Bob Chacha Wangwe alikuwa anakabiliwa na makosa ya kimtandao kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba ‘Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake, hivyo haitapata maendeleo kama itaendelea kunyanyaswa na kugandamizwa na Tanzania bara.

Ajiua kwa kuhusishwa na kashfa ya rushwa
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 16, 2017