Mgombea wa urais kupitia upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amedai kushinda katika uchaguzi wa rais na kukataa matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi yanayoonyesha Rais Museveni anaongoza katika kinyang’anyiro hicho.

Bobi Wine amesema kuwa uchaguzi wa nchi hiyo ulikumbwa na udanganyifu na wizi wa kura ambao haukuwahi kushuhudiwa katika histora ya Uganda

Kauli hiyo ameitoa leo hii Januari 15 alipozungumza na waandishi wa habari

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2020

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 38 hakutoa maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo, ambazo zinatofautiana na kauli ya serikali iliyotolewa Alhamis jioni kwamba uchaguzi umekuwa wa amani.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Simon Byabakama, aliwahakikishia Waganda  kwamba matokeo ya uchaguzi yamewasili kwenye kituo cha taifa cha kuhesabia kura licha ya kutokuwepo huduma ya Intaneti.

Rais Museven ambaye ameiongoza Uganda kwa takribani miaka 35 hajatoa kauli yoyote hadi kufikia sasa.

Mitaa ya jiji kuu la Kampala ilikuwa kimya hii leo, huku maduka mengi yakiwa yamefungwa. Wanajeshi wameendelea na doria kwenye mitaa mbalimbali. 

Matumaini mapya Saratani ya Mlango wa Kizazi
Messi akwaa kisiki Hispania