Kiungo Mkongwe nchini, Haruna Moshi maarufu ‘Boban’ amesema kuwa kitendo cha msemaji wa zamani wa Yanga, Jerry Muro kuponda uwepo wake ndani ya Yanga ni kumkosea heshima yeye, familia yake na klabu kwa ujumla.

Akiongea baada ya mchezo wa 16 bora ya kombe la shirikisho nchini (ASFC), ambapo Yanga ilishinda 1-0 dhidi ya Namungo FC, Boban amesema maneno hayo hayajamfurahisha hata kidogo na sio ya kimichezo kabisaa.

”Haya ndio matatizo ya mpira wetu, hatuendelei kwasababu tunachukua watu wa nje ya mpira na kuwapa dhamana ya kuongoza, kiukweli sijui alikuwa anafikiria nini kusema hivyo ila amenikosea sana mimi na familia yangu pamoja na timu yangu”, amesema Boban

Aidha, Boban alisajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili mwezi Disemba 2018, ambapo hadi sasa katika mechi 8 alizocheza, ameshahusika katika mabao zaidi ya manne hivyo kuwa na msaada katika timu hiyo ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu.

Hata hivyo, mapema wiki iliyopita mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro alisema wachezaji Mrisho Ngassa na Haruna Moshi wamezeeka na hawakuwa na haja ya kusajiliwa Yanga.

Kadinali Kanisa Katoliki akutwa na hatia ya kuwabaka wavulana
Makonda ajitwisha zigo, sasa kuinusuru Taifa Stars