Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina ‘Bobi Wine’ amekamatwa tena muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini humo.

Muda mfupi baada ya kuachiwa huru, Bobi Wine alikamatwa tena na imearifiwa kuwa anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Aidha, mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini humo leo alifikishwa katika mahakama ya kijeshi iliyopo mjini Gulu Kaskazini mwa Uganda.

Hata hivyo, Mawakili wake awali walitaarifiwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa jijini Kampala.

 

 

Makala: Kwanini Nikki wa Pili anaweza kuwa Rais, kwanini hawezi
Mtanzania anayemiliki mkoba wa gharama zaidi duniani ''Milioni 60''