Serikali ya Uganda imemuondolea mashtaka Msanii na mwanasiasa wa upinzani Uganda, Kyadondo, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine na muda mfupi baadae amekamatwa tena na anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini na wabunge wengine waliokamatwa.

Bobi Wine ameondolewa mashtaka ya umiliki haramu wa silaha yaliyokuwa yanamkabili mahakama ya kijeshi nchini Uganda.

Uamuzi huo unadhaniwa kushinikizwa na hatua ya jumuiya za kimataifa zilizoishinikiza serikali ya Uganda kumuachia huru Bob Wine.

Kabla ya Serikali ya Uganda kutangaza kumuondolea mashitaka Bob Wine, mawakili wake walijuzwa kuwa kesi ya mwanasiasa huyo machachari itasikilizwa katika kambi ya Kijeshi ya Makindye alikokuwa anazuiliwa Bob Wine.

Aidha, Bob Wine amepewa masharti magumu ya dhamana kulingana na umarufu wake anapopita mjini anakuwa na wafuasi wakubwa wakimfuatilia, na katika masahriti hayo amekatazwa kuhusika katika mkusanyiko au Maandamano kama anavyosema wakiri wake Asumani Basalilwa.

 

Rais Magufuli akemea mapenzi vyuoni, 'Haiwezekani ukumbatie bila kutoa mahari'
Ujumbe wa mwisho Mengi alioandika kwa mke wake na Watanzania