Msanii wa muziki nchini Uganda, Bobi Wine amemshukia vikali rapa kutoka nchini Marekani, Kanye West baada ya kukutana na Rais wa Taifa hilo Yoweri Museveni.

Amesema kuwa Kanye amejidhalilisha sana kwa kukutana na Rais Museveni, Jumatatu ya wiki hii katika Ikulu ya nchi hiyo.

Aidha, Bobi Wine amesema kuwa lingekuwa jambo kubwa sana kama angetumia muda wake kutangaza viongozi wazuri barani Afrika lakini sio kukutana na Rais mwenye miaka 32 madarakani, anayeminya Demokrasia na kukandamiza vyama vya upinzani.

“Pata picha mimi ni msanii lakini leo hii nazuiliwa kufanya tamasha ndani ya nchi yangu, kisa napingana na mawazo ya Rais halafu leo yeye anaenda kusalimiana naye,“amesema Bobi Wine alipokuwa akifanya mahojiano na Gazeti la The Guardian.

Hata hivyo, Kanye West na uongozi wake amekuwa nchini Uganda tangu wiki iliyopita akikamilisha baadhi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye albamu yake mpya ya YANDHI.

 

Mtoto mwenye utata wa jinsia apokelewa Muhimbili
Hakuna wa kuning'oa CUF- Sakaya