Mwamauziki wa Uganda aliyegeuka kuwa mwanasiasa, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kwa jina la ‘Bobi Wine’ amepigwa na vikosi vya usalama na hawezi kuzungumza wala kutembea

Mbunge huyo wa upinzani amefikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi katika mji wa Gulu uliopo kaskazini mwa nchi hiyo, ambako ameshtakiwa kwa makosa mawili ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na shtaka moja la kukutwa na silaha, lakini sio uhaini kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Aidha, Bobi Wine alikamatwa baada ya gari lililokuwa kwenye msafara wa rais Museveni kushambuliwa Jumatatu katika mji wa Arua.

Hata hivyo, Serikali ya Uganda haijatoa tamko lolote kuhusu tuhuma kwamba Bobi Wine alishambuliwa akiwa kizuizini.

 

Rungwe ‘aamsha’ na waliohama vyama, atabiri ya 2020
Video: Lissu ainyooshea kidole Chadema, Mume amuua mke kwa mundu, auawa