Mbunge na mwanamuziki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu, Bobi Wine amesema mapema leo atawasilisha rasmi barua katika Jeshi la Polisi nchini humo kuwafahamisha kuhusu maandamano yake ya amani kupinga kuzuiwa  vyanzo vyake vya mapato.

Bobi Wine ameeleza kufanya hivyo kufuatia kitendo cha kuzuiwa kufanya tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo kudhibiti maelfu ya mashabiki wake.

Amesema Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni anataka kuwazuia wanamuziki wote ambao hawamuungi mkono.

‘Rais Museveni amewaagiza Polisi kuzuia matamasha yangu kwa sababu hapendi kusikia ninachokiimba. Alitaka mimi niwe kama baadhi ya wasanii wanaoimba nyimbo za kumsifu na nilipokataa akaamua kuwa hataniruhusu kufanya onyesho lolote la muziki wangu nchini Uganda,’’ amesema Bobi Wine.

Msanii huyo ambaye pia ni mbunge wa upinzani, alikamatwa jana na kuzuiwa kwa saa kadhaa baada ya kupanga kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu  hatua ya Serikali kumzuia kufanya tamasha lake la Pasaka.

Wananchi wa Mtulingala wajenga Zahanati ya Kijiji
Video: Hizi ndizo Filamu 10 za kutisha zaidi Duniani | Huwezi kuangalia ukiwa peke yako

Comments

comments