Mbunge wa jimbo la Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi  maarufu kama ‘Bob Wine’ na wabunge wengine watatu wameachiwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo tarehe 27 Agosti, 2018 na Jaji wa Mahakama Kuu Steven Mubiru.

Aidha, Wabunge hao watatu waliokuwa wakizuiliwa kwa takribani wiki mbili wameachiwa huru pamoja na watuhumiwa wengine nane.

Hata hivyo, washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.

Rapa Swae Lee apasuliwa mdomo akiwa jukwaani
Benitez awapoza mashabiki