Wekundu wa Msimbazi Simba hii leo walikua na kibarua cha kucheza ugenini katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Njombe Mji katika uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Simba ambao hawakucheza ligi tangu walipokua katika maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Ala- Masry, hii leo wamerejea tena kwa kishindo, baada ya kusambaratisha Njombe Mji FC kwa kuibanjua mabao mabao mawili kwa sifuri.

Simba wamepata ushindi huo wa mabao mawili kupitia kwa nahodha na mshambuliaji wao hatari John Bocco katika dakika ya 17 na 64.

Ushindi huo unaendelea kuiweka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa kufikisha point 49, na kuwaacha mahasimu wao katika soka la bongo Young Africans wakiwa na point 46.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 4, 2018
Teknolojia ya kuwakumbusha wagonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu yavumbuliwa

Comments

comments