Wekundu Wa Msimbazi Simba hii leo walikua uwanjani kuendeleza kampeni yao ya kulisaka taji la ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu wa 2017/18, kwa kucheza na maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Priosns) kutoka jijini Mbeya.

Mchezo huo uliunguruma katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na kushuhudia wekundu hao wakiendelea kutakata kwa kukusanya alama tatu muhimu ambazo zinaendelea kuwasafishia njia ya kuelekea kwenye ubingwa.

Simba wanaongoza msimamo wa ligi kwa kipindi kirefu, wamepata ushindi wa mabao mawili kupitia nahodha na mshambuliaji wao John Rafael Bocco aliyefunga katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza, na bao la pili likawekwa kimiani dakika ya 80 na Emmanuel Okwi kwa mkwaju wa penati, iliyosababishwa na Bocco baada ya kuangushwa katika eneo la hatari.

Beki Jumanne El Fadhili, alilazimika kuonyeshwa kadi nyekundu iliyoambatana na kadi mbili za njano, kufuatia makosa ya kumuangusha kwa makusudi Bocco ambaye alikua naelekea kumsabahi mlinda mlango Aron Kalambo.

Ushindi huo unaiwezesha Simba kufiisha alama 58 na kuendelea kuwacha mahasimu wao wakubwa hapa nchini Young Africans wakiwa na alama 47 huku wakiwa na michezo miwili mkononi.

Michezo mingine ya ligi kuu ya soka Tanzania bara iliyochezwa hii leo ilikua kati ya Ruvu Shooting waliokua wageni wa Ndanda Fc kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na Kagera Sugar waliwaalika ndugu zo kutoka mkoani Morogoro Mtibwa Sugar.

Mkoani Mtwara mchezo kati ya Ndanda Fc dhidi ya Ruvu Shooting umekamilika kwa wenyeji kukubali kuchabangwa mabao matatu kwa moja.

Katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Kagera Sugar walimaliza dakika 90 za mpambano wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kulazimishwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Mkojo wa Sungura wageuka dili mkoani Njombe
Morocco kukaguliwa kwa fainali za dunia 2026