Mabingwa wa soka Afrika mashariki na kati Azam FC, watalazimika kuifunga Young Africans ili kujihakikishai nafasi ya kufuzu katika hatua ya mtoano ya Kombe la Mpinduzi.

Hiyo inatokana na matokeo ya mchezo wao wa jana baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba.

Hata hivyo, John Bocco ambaye ni nahodha wa Azam FC, amesema kazi ni ngumu kwa kuwa Young Africans ina kikosi bora na chenye ushindani mkubwa.

“Tunawaheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa. Tunajua nasi ni timu kubwa na bora, itakuwa mechi ngumu sana.

“Lakini tunaiweka kando mechi ya Jana na tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo kujiandaa dhidi ya Yanga,” alisema nahodha huyo aliyedumu kwa muda mrezi Azam FC.

Kabla ya kukutana na Azam FC, Jamhuri ilikuwa imekutana na dhoruba ya kipigo cha mabao sita kutoka kwa Young Africans.

Wilfred Ndidi Anukia King Power Stadium
Watumishi wa umma wawezeshwa kupata nyumba