Bodi ya Filamu nchini Kenya (KFCB) imeipiga marufuku filamu iitwayo ‘Rafiki’ inayogusia masuala ya mapenzi ya jinsia moja.

Filamu hiyo ni ya kwanza kutoka Kenya kuchaguliwa ili kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la Cannes mwaka huu.

KFCB imepiga marufuku filamu hiyo kuonyeshwa hadharani au kutangazwa kwenye televisheni na kusambazwa, ikisema kuwa maudhui ya filamu hiyo inayoonyesha mapenzi ya jinsia moja, inakiuka sheria za Kenya.

Aidha, Bodi hiyo imeonya kuwa mtu yeyote atayekutwa na filamu hiyo atachukuliwa hatua za kisheria, huku wanaharakati wanaotetea mapenzi ya jinsia moja waliandika kwenye mtandao wa Twitter wakiishutumu bodi hiyo.

Hata hivyo, mwezi Juni mwaka jana, Bodi hiyo ilipiga marufuku baadhi ya vipindi vya televisheni katika ving’amuzi vya DSTV na GOTV vilivyosemekana kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja.

 

 

Mashabiki, Wanachama wa Simba waombwa kufika Taifa
Uganda yaomboleza kifo cha Sokwe