Uchaguzi mdogo wa kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kujaza nafasi zilizo wazi utafanyika Jumamosi Novemba 17, 2018 jijini Dar es Salaam.
Fomu kwaajili ya Wagombea zitaanza kutolewa Septemba 21,2018 kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni saa 10 kamili jioni Septemba 25,2018.
Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Kuu (PL)L,Mjumbe mmoja kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL).
Ada ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti ni sh.200,000(Shilingi laki mbili)mbili wakati nafasi nyingine zilizobaki ni sh.100,000(Shilingi laki moja).
Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
Wagombea kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ni marais au Wenyeviti wa Klabu husika, Hivyo, Wagombea wanatakiwa kuwa Wenyeviti au Marais wa Klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB inagombewa na Klabu za Ligi Kuu pekee.

Cape Verde waanika rasmi tarehe ya kuikabili Taifa Stars
Douglas Costa awaomba radhi mashabiki, wachezaji