Siku moja baada ya kutangaza tarehe mpya za baadhi ya michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, bodi ya ligi imetoa taarifa nyingine za mabadiliko zinazouhusu mchezo namba 199 kati ya Mbeya City na Young Africans uliokua umepangwa kufanyika Mei Mosi, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Taarifa kutoka bodi ya ligi inaeleza kuwa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine ili kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mchezo mmoja na mwingine isiwe chini ya angalau saa 72.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara inaonyesha kuwa, Young Africans watakua na mchezo dhidi ya Simba utakayofanyika Aprili 29 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mbowe na viongozi wake waswekwa mahabusu
La Pulga kuivaa Hispania Wanda Metropolitano stadium

Comments

comments