Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Mwezi Januari hadi Machi mwaka huu imekusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 132 kutoka kwa wadaiwa.

Kutokana na kiasi hicho kukusanywa kutoka kwa wadaiwa ambao ni wanufaika wa mikopo, bodi hiyo imefanikiwa kuvuka lengo la kiasi cha Tsh. Bilioni 130 iliyokuwa imejiwekea.

Aidha, akitoa taarifa hiyo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo, Fidelis Joseph amesema lengo limefikiwa na kuvukwa kutokana na ushirikiano wa wote (Bodi na wadaiwa).

Hata hivyo, amewakumbusha wadaiwa kulipa deni kwa wakati maana kuna ongezeko la 6% kwa mwaka tangu anaanza kupatiwa mkopo hadi anapomaliza kulipa deni. Pia kuna penati kwa watakaochelewa.

 

 

 

Putin aapishwa urais Russia
Bunge lawahakikishia huduma nafuu Waislam mwezi wa Ramadhan