Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu HESLB, imesema huwa inatoa taarifa kwa wastaafu ambao wanadaiwa na bodi hiyo, ili walipe mikopo yao wanayodaiwa kwa utaratibu wa kawaida kukinusuru kiinua mgongo chao kisikatwe bila utaratibu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo nchini, Fidelis Joseph katika kipindi cha East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio, wakati akizungumzia hali ya urejeshaji wa mikopo kwa wanafunzi ambao walikuwa wanufaika.

“Taratibu za kuwafuata wastaafu ni wa kawaida sana, hatusemi tunaenda kuchukua kiinua mgongo chake chote, ila tunampa taarifa kuwa anadaiwa, kwa hiyo atakuwa anajukumu la kulipa, deni litaisha pale utakapokuwa umekufa, au matatizo ya kudumu kama ugonjwa, kwa hiyo kama ni mstaafu lazima ulipe hili deni kwa njia yeyote.”amesema Joseph

Aidha, kuhusiana na ongezeko la deni la bodi hiyo kwa wanafunzi kila mwaka kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya walionufaika, Fidelis amesema wamewekewa sheria ambayo lengo lake ni kulinda thamani ya fedha kwa watu ambao wanachelewesha.

“Madeni ya Serikali hayana riba ila yana tozo ili kulinda thamani ya fedha, mfano kama ukidaiwa milioni 10 unadaiwa milioni 10.6 na kama ulilipa milioni 5 ukifika mwisho wa mwaka unadaiwa asilimia 6 ya milioni 5, lengo lake ni kweli kwamba kwa sababu hela huwa inabadilika thamani lakini si kweli kwamba deni la bodi huwa haliishi.”, ameongeza Joseph

Balozi wa China nchini Uingereza ahojiwa
Rais alaani ‘jaribio la mauaji ya halaiki’