Bodi ya Wadhamini wa Young Africans imesistiza uchaguzi wa klabu hiyo utafanyika Juni 5, mwaka huu na si Juni 25, kama ambavyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeagiza.

Taarifa ya Bodi ya Wadhamini ya Yanga imesema kwamba hawawezi kuchelewa kufanya uchaguzi kwa sasa kwa sababu mbalimbali za msingi.

Kwanza, timu ipo kwenye mashindano ya Kombe ya Afrika, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).

Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba viongozi wapya wa Yanga wanatakiwa kuingia madarakani mapema ili waanze kufanya usajili na kupanga mambo mengine ya msimu mpya.

Aidha, Bodi hiyo pia imepinga uchaguzi wao kusimamiwa na TFF – badala yake imeagiza usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya klabu na TFF watakuwapo kama waangalizi.

“Yanga imesajiliwa kama CCM, CUF, CHADEMA lakini tofauti ni wengine wamesajiliwa kama vyama vya siasa, Yanga imesajiliwa kwa ajili ya michezo na Mamlaka ya Michezo chini ya Wizara ya Michezo na Utamaduni, na katika michezo hiyo ukiwemo mpira wa miguu, imejisajili yenyewe TFF,”.

“Kwa maneno mengine, Yanga ingeweza kuchagua kushiriki Netiboli ingejisajili na Shirikisho la Netiboli, na au michezo mingine, kama ngumi ingejisajili Shirikisho la Ngumi, lakini kwa kujisajili kwenye soka haiwazuii kufanya mambo kwa mujibu ya Katiba yao,” imesema taarifa hiyo.

Hans Pope Amshangaa Jerry Muro Kulivimbia Suala La Rushwa
Wabunge waugomea utaratibu wa ofisi ya Bunge, wadai sio wanafunzi