Wakati Nigeria ikiomboleza miaka minne tangu kutekwa kwa wanafunzi wa kike wa eneo la Chibok, UNICEF imeripoti kuwa zaidi ya wasichana 1000 wametekwa tangu mwaka 2013 hadi leo na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Boko Haram wamekuwa wakivamia shule hasa za bweni na kuteka wanafunzi wa kike.

“Tangu mwaka 2013, zaidi ya wanafunzi 1000 walitekwa na Boko Haram kaskazini mwa Nigeria, wakiwemo wasichana 276 wa shule ya sekondari mjini Chibok mwaka 2014,” imeeleza taarifa ya UNICEF.

Muwakilishi wa UNICEF, Mohamed Malick amesema kuwa mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya wanafunzi wa kike hayavumiliki.

Boko Haram inaendesha mapigano kujaribu kuweka utawala wa kidini katika eneo la kaskazini mwa Nigeria.

Kundi hilo linapinga elimu yenye muelekeo wa elimu ya Magharibi kwa hasa kwa wasichana.

Kwa mujibu wa UNICEF, zaidi ya walimu 295 wameuawa na Boko Haram na zaidi ya shule 1400 zimeharibiwa na kundi hilo tangu mwaka 2009.

Serikali ya Nigeria imeendelea kupambana na kundi hilo na mara kadhaa imekuwa ikitangaza kuwa imelisambaratisha, lakini huibuka na kufanya mashambulizi katika maeneo ya jeshi la nchi hiyo na makaazi ya raia.

Video: Rihanna ndani ya mchezo wa wizi kwenye ‘Ocean’s 8’
Mwakyembe asubiriwa kuwahukumu Nandy na Bill Nas