Wapiganaji wa Boko Haram Nchini Nigeria, wamevamia Kambi moja ya Kundi Hasimu linalojiita Dola ya Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP) na kusababisha mapigano makali ya risasi ambayo yalisababisha vifo vingi.

Wapiganaji wa Boko Haram waliishambulia Kambi ya Kijiji cha Sunnawa katika Wilaya ya Abadam karibu na mpaka na Niger.

Mapigano makali ya kufyatuliana risasi kati ya makundi mawili hayo ya Kigaidi Kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha wapiganaji wengi kuuawa.

Wanamgambo wa Kundi la ISWAP awali waliwavamia Boko Haram katika eneo la Diffa huko Niger lilipoko jirani ya Nigeria ambako waliwateka nyara wanawake 13.

Misururu yayeyuka usajili wa laini, Mjerumani akutwa amekufa hotelini Z'bar
Idadi wasioajiriwa yaongezeka lukuki, vijana wafikia milioni 267

Comments

comments