Bwana harusi Mohammed Hassan na mpambe wake, Bogale Sebsibe wamepoteza maisha baada ya bomu la kurushwa kwa mkono alilokuwa amelificha kulipuka.

Kwa mujibu wa BBC, marafiki hao walikuwa katika harakati za kujiunga na sherehe ya kimila ya fungate la siku kumi, ambapo mpambe wa bwana harusi hupewa nafasi ya kuwaburudisha maharusi wapya.

Tukio hilo lilitokea kijijini, katika eneo Kanda ya Wollo mkoani Amhara, Kaskazini mwa jiji la Addis Ababa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wilaya ya Borena, Nigatu Tameme, bwana harusi alikuwa anamiliki bomu hilo kinyume cha sheria.

Kwa bahati, bibi harusi hakuwepo katika eneo hilo wakati bomu linalipuka kutoka kwenye mfuko wa bwana harusi huyo.

Mamlaka nchini Ethiopia imekuwa ikifanya oparesheni maalum kwa lengo la kutokomeza umiliki wa silaha kinyume cha taratibu.

Kadhalika, imeweka marufuku kwa watu ambao hufyatua risasi hewani wakati wa sherehe za harusi au misiba.

Kesi ya Mauaji Mwanafunzi Spelius yasikilizwa kwa mara ya kwanza
Daladala zatakiwa kupisha ujenzi wa miundombinu kituo cha Gerezani