Wakazi wa visiwani Zanzibar jana walipatwa na taharuki baada ya bomu lililogundulika likiwa limetengwa katika kituo cha polisi cha Mkunazini kuteguliwa na kulipuliwa.

Ripoti kutoka visiwani humo zilieleza kuwa taarifa za kuwepo kwa bomu hilo zilitolewa na ‘wasamalia wema’ waliokuwa waliokishtukia kitu kilichukuwa kimewekwa kwenye mfuko wa plastiki kikiwa na muonekano wa simu ya mkononi.

Jeshi la Polisi liliwasiliana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao walifika na kuthibitisha kuwa kitu kile kilikuwa bomu kabla hawalitegua kwa kukata waya zilizokuwa zimeunganishwa na kisha kulilipua, hali iliyozua taharuki na kuwafanya wananchi kukimbia hovyo kwa hofu.

Eneo la Darajani liligeuka uwanja wa mbio zisizo rasmi na kelele za wananchi walioingiwa hofu, huku barabara kadhaa zikifungwa kwa sababu za kiusalama.

Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam na kueleza kuwa bomu hilo halikuweza kuleta madhara yoyote kwa binadamu kwa kuwa liligundulika mapema na kuteguliwa japo lililipuliwa.

Tukio hilo lilizua taharuki zaidi hasa kufuatia hali ya kisiasa iliyopo hivi sasa visiwani humo baada ya Mwenyetiki wa ZEC kutangaza kufuta uchaguzi huo, huku mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akipinga uamuzi huo na kushikilia msimamo wake kuwa Tume hiyo iendelee na utaratibu wa kuhakiki matokeo kutoka vituoni na kumtangaza mshindi.

Viongozi Wa Ukawa Waibukia Uholanzi..
Kevin MacDonald Arejesha Vijembe Kwa Mahasimu