Bondia wa Uingereza, Scott Westgarth amefariki dunia kutokana na maumivu aliyoyapata katika pambano lake la Jumamosi ambalo alishinda kwa alama.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 31 alimshinda Dec Spelman lakini alipoenda kwenye mahojiano baada ya pambano hilo alionekana mwenye maumivu na baadaye kukimbizwa hospitalini.

Westgarth alikuwa anapambana kubeba mkanda wa ubingwa wa Uingereza. Rekodi yake ya mapambano inaonesha aliwahi kushinda mapambano sita, akapoteza mawili na kutoa sare moja.

Taarifa ya kifo chake iliyotolewa na promota wake ilieleza kuwa bondia huyo alikuwa kijana mdogo aliyekuwa akifanya kazi anayoipenda.

Mpinzani wake katika pambano la usiku huo, Spelman alitoa heshima yake na kuonesha kusikitishwa na kifo chake.

“Nimevunjika moyo na nimeishiwa maneno ya kusema. Nitaendelea kuiombea familia ya Scott na watu wake wa karibu. Pumzika salama rafiki yangu,” aliandika.

Kibatala kukata rufaa, Wasanii wafunguka hukumu ya Sugu
Shyrose akanusha kumponda JPM

Comments

comments