Bondia Amir Khan amekiri kwamba hana nguvu za kumjeruhi Saul Canelo Alvarez katika mpambano wao wa kuwani ubingwa wa WBC uzani wa kati, utakaofanyika mjini Las Vegas nchini Marekani siku ya Jumamosi.

Khan ambaye ni raia wa nchini England amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesisitiza kasi yake kupambana ndio itakayomuwezesha kuibuka kidedea katika pambano hilo.

”Nitampiga Canelo na huenda asisikie ngumi zangu lakini ujuzi ndio utakamshinda”,alisema Khan.

”Sitaki kushiriki katika kurushiana makonde, kusimama mbele yake na kumpa fursa ya ya kuinipiga”,ninajua anaweza kuniumiza na ngumi moja kali.

”Kwa hivyo lazima niwe chonjo nitakaporusha ngumi zangu. Ni nidhamu na kuhakikisha kuwa ninaendelea na mpango wangu wa mechi hiyo hadi raundi ya 12”.

”Mbeleni, sikuwaheshimu mabondia ambao wamenibwaga sakafuni. Pambano hili najua naweza kujeruhiwa kwa hivyo nitakuwa chonjo na kujilinda”.

”Pambano dhidi ya Mayweather au Manny Pacquiao lingekuwa rahisi kwangu kwa sababu tuko sawa kwa urefu kwa hivyo ningekuwa na nguvu kimwili.Canelo atakuwa na nguvu lakini vitu nilivyojihami navyo ni kasi na mwendo”.

Zimbabwe kutoa Dola yake yenye thamani sawa na Dola ya Marekani
Snura hana majanga na chura wake, awapa neno mashabiki