Bondia Amir Khan, ametangaza kuwa tayari kusaidia janga la wakimbizi wanaoendelea kuingia katika baadhi ya nchi za barani Ulaya wakitokea sehemu mbali mbali za dunia.

Khan amesema ameumizwa na janga hilo ambalo limekua likichukua nafasi siku hadi siku na vyombo vya habari vimekua vikionyesha athari zake huku wengine wakipoteza maisha baharini.

Amesema msaada anaodhamiria kuutoa atauelekeza kwa wakimbizi waliopo nchini Ugiriki ambao wamekua wakiingia kwa wingi nchini humo wakitokea Syria ambapo kuna machafuko ya vita kwa zaidi ya miaka mitatu.

Jana jioni bondia huyo alitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuonyesha picha ya mkimbizi kutoka Syria aliyejulikana kwa jina Aylan Kurdi, ambaye alionekana amebeba mtoto aliyepoteza maisha baharini.

Mkimbizi huyo alionekana akiwa habarini, hali ambayo Khan ameielezea kama pigo kwa wanaadamu wenzake ambao wanaendelea kupata tabu kwa kukimbia machafuko katika nchi zao.

Khan mwenye umri wa miaka 28, amejinasibu kusafirisha mizigo kwa njia ya barabara ambayo itajumuisha nguo, viatu, mahema pamoja na vifaa vya matumizi ya lazima kwa bianadamu kama saguni, dawa ya meno, mafuta ya ngozi nk.

Kama itakumbukwa vyema Amir Khan, mwaka jana alijitolewa msaada kwa watoto 132 walioachwa wakiwa baada ya wazazi wao kuuawa huko Peshawar nchini Pakistan na kundi la Taleban.

Khan alilazimika kuuza bukta yake aliyokua imenakshiwa na madili ya dhahabu na pesa zilizopatika aliziwasilisha kwa ajili ya watoto hao.

Utafiti: Nani Mshindi Urais 2015?
Ufisadi Wa Jack Warner Waendelea Kudhihiri FIFA