Mtanzania kutoka Tanga, Bondia Hassan Mwakinyo leo ametembelea Bungeni Dodoma katika kikao chao cha mwisho  ambapo wabunge wameweza kumchangia T.sh 20,000 kwa kila mbunge kutoka kwenye posho zao na kufikisha Milioni 7.72 kama zawadi mara baada ya kuitangaza vyema Tanzania kimataifa alipoibuka na ushindi katika mchuano mkali uliomkutanisha na Bondia Sam Eggington wa Uingereza katika pambano lililochezewa Birmingham.

Hayo yamejiri baada ya Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hilaly kuomba mwongozo wa kwa wa Spika, Job Ndugai.

“Tumekuwa tukiwachangia sana mamisi humu ndani, leo hii tunaomba mwongozo wako angalau tumchangie Tsh. 20,000 kila mmoja, naomba mwongozo wako spika, alisema Aeshi.

Wabunge waliitika kwa makofi mengi kisha Spika Job Ndugai alipitisha mwongozo huo mara moja kila mbunge atakatwa posho yake.

Mwakinyo alimtwanga Eggington ambaye aliwahi kuwa Bondia namba moja wa Uingereza sekunde ya 45 ya mzunguko wa pili wa mchezo huo na kutangazwa Bingwa.

Aidha, Wabunge wamemtakia Hassan Mwakinyo mafanikio mema katika michuano inayoendelea na kumsihi aendelee kuiwakilisha vyema Tanzania kimataifa ili kuijengea nchi heshima.

Serikali mkoani Simiyu kutoa ardhi bure kwa wawekezaji
Q Jay apandwa kichaa, Makamua afunguka

Comments

comments