Bongo muvi  inafanya vizuri katika tasnia ya Filamu, na hii imedhirishwa wazi kwani baadhi ya muvi za kibongo sasa zinaanza kuoneshwa katika majumba ya sinema (cinemax).

Katika hali ya kawaida imezoeleka kuwa sinema zinazotengenezwa nje ya Tanzania zinauuza ziadi katika majumba ya Sinema, kwani hata wamiliki wa majumba hayo  ya starehe hutumia zaidi sinema za kigeni kuuza na kukuza biashara yao.

Dhana hii imetengenezwa na sisi wenyewe watanzania kwa kuthamini na kuamini vipaji vya wasanii wa nje na kuacha kusapoti nguvu kazi ya wasanii wa ndani.

Hivi karibuni mmoja ya Mtanzania aliyejikita zaidi katika maswala ya sanaa na uigizaji baada ya kipaji chake kuonekana mbele ya macho ya wengi na kupewa urais wa kuongoza kampuni ya filamu huko Marekani, Ernest Napoleon sasa amekuja na hii mpya ”Kiumeni”.

Ernest Napoleon, ameingia mkataba na mchekeshaji, Idriss Sultan na kutengeneza filamu iitwayo ”Kiumeni”. kutokana na ubora wa filamu hii, Idris Sultan ametangaza rasmi machi 17 mwaka filamu hiyo itaoneshwa katika nyumba ya sinema Mlimani City.

Hivyo Sultan aliomba sapoti toka kwa watanzania kujitokeza siku hiyo ili kushuhudia vijana walivyojipanga katika kuboresha tasnia ya Bongo Muvi.

Idriss Sultani ameandika katika akaunti ya instagram ”17 March cinemax mlimanii city kama vipi kaweke booking yako tu sasaivi mlimani city becouse TUNAJAZAAAA CINEMA LOTEEE ukikosa omba ya 18 ukikosa omba ya 18 ukikosa omba ya 19 #kiumenimovie”.

Filamu za kibongo kuoneshwa cinemax Mlimani city
Samson Siasia Ana Ndoto Za Kuzinoa Afrika Kusini, Rwanda