Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amemtaka Waziri wa Maji, Isaack Kamwelwe kuweka wazi mahali zilipo dola milioni 500 kutoka Serikali ya India ambazo waliahidi kwa ajili ya miradi ya maji kijijini.

Ameyasema hayo Bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, ambapo mbunge huyo ameshangazwa kuona mpaka hata kijijini kwa Mwalimu Nyerere hakuna maji.

“Waziri ulituambia kuna dola milioni 500 za serikali ya India kwa ajili ya maji vijijini utueleze ziko wapi. kama mmesahau sisi wengine tuna kumbukumbu. yaani hata kwa Mwalimu Nyerere hakuna maji? Nimezaliwa Tarime kuna maji, lakini kadri tunavyozidi kwenda mbele tunarudi nyuma, ndiyo maana tunasema bora wakoloni kuliko serikali ya CCM,”amesema Heche

Hata hivyo, Pamoja na hayo Mbunge huyo amesema hata suala la kuundwa tume kutokana na miradi ya maji kukwama limewahi kujadiliwa mara nyingi lakini ni kama linapigwa danadana.

 

 

Video: Serikali yacharuka sakata la mafuta ya kula, Dawa kinga ya Ukimwi yazinduliwa
Magazeti ya Tanzania leo Mei 10, 2018