Klabu ya Borussia Dortmund imesalimu amri kwa kukubali kumuweka sokoni kiungo kutoka nchini Armenia Henrik Mkhitaryan.

Klabu hiyo ya Westfalenstadion imefikia hatua hiyo, baada ya zoezi la kumshawishi Mkhitaryan kusaini mkataba mpya kushindikana, na suluhisho limeonekana ni bora aingizwe katika orodha ya wachezaji watakaoondoka katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika gazeti la Daily Mirror, Borussia Dortmund wametangaza rasmi kuwa tayari kupokea ofa ya klabu yoyote ambayo itakua radhi kumsajili Mkhitaryan.

Taarifa za gazeti hilo zimeendelea kutanabaisha kwamba, klabu ya Arsenal tayari imekuwa ya kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

Hata hivyo imeelezwa kwamba, Arsenal bado hawajawasilisha ofa ya usajili wa kiungo huyo ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine kuanzia mwaka 2010–2013.

Wakati Henrik Mkhitaryan akiwekwa sokoni, tayari uongozi wa Dortmund umeanza mikakati ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Mexico, Jurgen Damm, ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Tigres UANL.

Vutankuvute: CCM kuing'oa miba ya Chadema kuhusu Magufuli kila kona
Jose Mourinho Apongezwa Kwa Mipango Ya Usajili Wa Bailly