Adhabu ya kufungiwa kusajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, imeanza kuigharimu klabu bingwa duniani (Real Madrid) baada ya kushindwa kufanikisha usajili wa kinda kutoka nchini Sweden Alexander Isak.

Real Madrid walionyesha nia ya kumsajili kinda huyo kwa kipindi kirefu, na waliamini huenda wangefanikisha kumpata, endapo wangeshinda  rufaa ya kupinga adhabu ya kusajili waliyoiwasilisha kwenye mahakama ya kimichezo CAS mwishoni mwa mwaka jana.

Taarifa zinaeleza kuwa, klabu ya Borussia Dortmund imefanikisha azma ya kumsajili Alexander Isak mwenye umri wa miaka 17, akitokea AIK Fotboll.

Kiasi cha Pauni milioni 8.65 kimetajwa kutumika katika uhamisho wa mchezaji huyo, ambaye anatarajiwa kuwa mrithi wa Zlatan Ibrahimovic, kutokana na uwezo wake wa kusakata soka.

Jana Isak alisafiri kuelekea nchini Ujerumani, kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kujiunga na Borussia Dortmund.

Kwa msimu huu wa 2016/17, Isak aliitumikia klabu ya AIK Fotboll katika michezo 24, na tayari ameshacheza michezo miwili na kufunga bao moja akiwa na timu yake ya taifa Sweden.

Majimaji FC Kumsubiri Mshindi Wa Mighty Elephant Vs Shujaa FC
Mtanzania Ernest Napoleon, ateuliwa urais wa kampuni ya filamu Marekani